Kupitia jukwaa hili (www.lawimshana.com) utajengewa uwezo kiroho, kimahusiano, kiakili na kiuchumi na kuunganishwa na majukwaa mengine ya mtandaoni kama vile Facebook, Tiktok na Youtube. Mungu amempa Dkt. Lawi Mshana wito wa kujengea uwezo watu binafsi na jamii kupitia warsha, makala, vitabu, video na audio. Walengwa wakuu ni viongozi, wajasiriamali, wanandoa, vijana na watu wanaoishi katika mazingira hatarishi. Anashirikiana kwa karibu na mke wake pamoja na watumishi mbalimbali.